JE UNAMPENDA ALIYEPENDWA?FANYA YAFUATAYO

Habari zenu wakuu!!
leo tuzungumzie kumpenda aliyependwa, Kupenda hakuna macho! Moyo ukishapenda hausikii wala kuambiwa. Katika hili ndiyo maana unaweza kumuona mwanaume kazimika kwa msichana ambaye hawaendani kabisa lakini moyo wake ndio umeshapenda. 
Hayo ndiyo mapenzi jamani!, mwanaume unaweza kujikuta unaangukia kwa msichana ambaye tayari ana mpenzi wake yaani ameshapendwa. Moyo wako unakuambia yeye ndiye mtu sahihi katika maisha yako lakini tayari ana mtu wake, unafanyaje?
Kuna mambo kadhaa ya kukusaidia kama yafuatayoo 
Kwanza… Chunguza 
Tumia muda wako mwingi kuchunguza juu ya uhusiano wake. Uhusiano wao umesimama na wanaonekana ni watu wenye ‘future’? Nasema hivyo kwa sababu, yawezekana uhusiano wa huyo uliyetokea kumpenda ni wa kuzuga tu na huenda wewe ndiye mwenye future naye. 
Pili… Usitafute uadui 
Baada ya kuchunguza, ukibaini kwamba uhusiano wao hauko ‘serious’, vuta subira, lolote linaweza kutokea na likaufurahisha moyo wako. Lakini kama utaona ni watu walio siriasi na wanaelekea kuoana, usitafute  uadui bure, kaa pembeni. 
Tatu… Una nafasi kwake? 
Sawa umetokea kumpenda msichana/Mvulana aliye na mtu wake, umeshawahi kujiuliza kama una nafasi ndani ya moyo wake? Anaonesha dalili fulani za kukupenda kama unavyompenda na ni mtu anayeonesha kukumisi 
anapokuwa mbali na wewe? Utakapobaini una nafasi kwake, uamuzi wa kumpotezea hautakuwa na nafasi. 
Nne… Ni rahisi kubadili uamuzi wake? 
Unadhani huyo uliyetokea kumpenda anaweza kubadili maamuzi ya kumuacha huyo aliyenaye kama kweli hawana ‘future’? Utagundua hilo kwa kuongea naye na kumsikia kama anaweza kufanya maamuzi hayo ili awe na wewe. 
Tano… Pingana na moyo wako
Ifike wakati upingane na moyo wako. Unajua moyo wako kukuambia kuwa unataka kuwa na uhusiano na mwanamke/mwanamme ambaye tayari ana mpenzi wake wakati mwingine utakuwa unakupotosha.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI NDIZO TOP 4 ZA STAILI ZA KUFANYA MAPENZI ILI KUKUSAIDIA USIKOJOE MAPEMA

JINSI YA KUMRIDHISHA (KUMLA SAWA SAWA)MWANAMKE KITANDANI

MASWALI UNAYOWEZA KUMUULIZA MPENZI WAKO KWA MARA YA KWANZA MNAPOKUTANA