HIZI HAPA SIFA ZA WIFE MATERIALS KWA KIJANA ANAYETAKA KUOA
Je wewe ni single boy? Au bachela kama wengi ambavyo hupenda kujiita? Kama jibu ni ndio basi naomba utambue ya kwamba suala la kupata mke si kazi bali kupata wife material ndio kazi. Hivi hujawahi kusikia wahenga wa zamani wakisema ya kwamba ni heri ukosea njia utauliza kwa pita njia kuliko ukosee kuoa? Hii ina maana gani? Hii ina maana ya kwamba wakati unafanya mchakato wa kutafuta mke wa kuoa ni lazima uzingatie misngi na mchakato mzima wa kupata mke bora na si ke bora.
Miongoni mwa misingi hiyo ni lazima uchagua mwanamke ambaye atakuwa na sifa hizi:
1. Mwanamke ambaye hana tamaa ya pesa.
Katika maisha ya sasa mwanamke anayependa sana pesa ukikubali awe mkeo mtasumbuana sana. Kwa maana hiyo mwanamke ambaye utagundua hana tamaa ya pesa, kwamba ikiwepo, ikikosekana anabaki kuwa yuleyule wa siku zote, huyu ni ‘wife material’.
2. Mwanamke anayependa watoto
Utajuaje kama mwanamke uliyenaye ana mapenzi na watoto? Iko hivi; katika uhusiano wenu ukiona ni mtu wa kupendapenda sana watoto wa marafiki zake, kuwanunulia zawadi, kuwashauri wenzake namna nzuri ya kuwalea watoto, hata akija kupata wa kwake itakuwa ni hivyohivyo, huyo ni wife material unatakiwa kumoa haraka.
3. Mwanamke ambaye ana heshima ya kweli.
Msichana ambaye anaheshimu kila mtu, mdogo na mkubwa, anawapenda na kuwaheshimu ndugu, jamaa na marafiki zako, huyu ana sifa ya kuwa mkeo pia.
Msichana ambaye anaheshimu kila mtu, mdogo na mkubwa, anawapenda na kuwaheshimu ndugu, jamaa na marafiki zako, huyu ana sifa ya kuwa mkeo pia.
4. Mwenye uwezo wa kujishusha.
Ogopa sana mwanamke ambaye anataka usawa, yaani yeye hata akikosea anakuwa hayupo tayari kusema samahani msichana wa aina hii hafaai bali Anayekufaa ni yule anayejua yeye ni mke, nawewe ni mume. Anayetambua kuwa, mwanaume ndiye kiongozi wa familia.

5. Mtu ambaye anakushauri kwenye mema.
Kama mpenzi wako ni wa kukutaka kila siku muende baa au mfanye madili hatari ili mpate pesa, huyu hana sifa ya kuwa mkeo. Mke ni yule ambaye atakuongoza kwenye kutenda mema na kuacha mabaya. Kwa mfano kama unakunywa pombe atakushauri uache, kama siyo mtu wa ibada, atakushawishi umjue Mungu wako na mambo mengine kama hayo

Comments
Post a Comment